WARDA BABY-WAAMBIE- OFFICIAL VIDEO FROM ZANZIBAR TANZANIA.

WAELEZE- Loly pop feat Chidi Short cut - OFFICIAL VIDEO from ZANZIBAR TA...

Arejeshwa Uingereza kwa kukiuka sheria Uganda, kwa Charles Nyangiti

Uganda imemrejesha nchini Uingereza mtunzi wa mchezo wa kuigiza kuhusu wapenzi wa jinsia moja ambao ulimeletea masaibu hata akakamatwa na kushtakiwa na polisi.
David Cecil alikamatwa kwanza mnamo mwezi Septemba kwa kuonyesha mchezo huo wa kuigiza bila ya idhini kutoka serikali ya Uganda.
Hata hivyo mashtaka dhidi yake yalitupiliwa mbali na mahakama kwa kukosa ushahidi wa kutosha.
Alikamatwa kwa mara nyingine wiki jana huku serikali ikiandaa mipango ya kumrejesha Uingereza, kwa misingi ya kuwa mtovu wa nidhamu. - kutoka Charles Nyangiti